Kama hujasoma Magazeti ya Leo Desemba 01 nimekuwekea hapa zile story kubwa zote.
MWANANCHI
Diwani Hassan Kijuu alijikuta
akiondolewa katika kikao cha Mkuu wa Mkoa na Watendaji wa Halmashauri,
Diwani huyo akisema kwamba Mkuu wa Mkoa ameanza vibaya na kumtuhumu kuwa
amekuwa akiwatisha Watendaji.
Amri ya kuondolewa Diwani hiyo kutoka
katika kikao hicho ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa
Mulongo baada ya kurushiana maneno ambapo Diwani huyo alipewa nafasi ya
kuzungumza kuhusiana na hatua ya ujenzi wa Maabara ilipofikia na Diwani
huyo akaanza kwa kumlalamikia Mkuu huyo wa Mkoa kwamba hawezi
kuzungumza habari za ujenzi wa Maabara wakati hajawaletea fedha.
Mulongo amewataka Watendaji hao kutoa
taarifa juu ya upotevu wa Bil. 40 katika Halmashauri hiyo kama ambavyo
imeonekana kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG
kuhusiana na upotevu huo.
MWANANCHI
Kituo cha afya Wilaya ya Bunda, Mara
kiko katika wakati mgumu ambapo kituo hicho wameshindwa kutoa pesa Benki
kiasi cha Sh. 3,139,590/- kutokana na wangehusika wote ambao walitakiwa
kutia saini kuwa wamefariki, japo Diwani wa Kata ya Bunda amesema kuwa
kiasi hicho cha pesa ni kidogo ukilinganishwa na hali ya uhitaji
iliyopo.
Mganga Mkuu wa Kituo hicho Charles
Mkomba amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa litamalizika
karibuni, kituo hicho kinategemewa na watu zaidi ya 120,000.
MWANANCHI
Wananchi wa Shinyanga wameshauriwa
kuacha tabia ya kumaliza kesi za kikatili wa kijinsia kienyeji na
kupelekea wahusika wa matukio hayo kutochukuliwa hatua za kisheria
Hayo yamesemwa na Rachel Madundo ambaye
ni mraghibishi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa katika Wilaya hiyo kwenye
maadhimisho ya 16 ya siku ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Aidha amesema kuwa sababu inayopelekea
kesi hizo kumalizwa kinyemela ni kutokana na kupewa rushwa huku idadi ya
kesi zilizowahi kuripotiwa kuanzia Januari mpaka Oktoba kuwa ni nne tu
kati ya 50 zinazohusu ukatili wa kijinsia.
TANZANIA DAIMA
Ajali mbaya imetokea Tanga ambapo watu
saba wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya
Mitsubishi Canter yenye namba T 783 BLM majira ya saa 11:00 jioni siku
ya jana.
Kamanda wa Polisi Tanga Fressar Kashai
alisema gari hilo lilitokea kijiji cha Ambangulu kwenye sherehe ya
harusi na kupinduka likiwa njiani, chanzo chake hakijafahamika na dereva
wa gari hilo Ramadhan Omar anashikiliwa na Polisi.
NIPASHE
Baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitisha maazimio kadhaa mwisho wa wiki iliyopita, imeonekana
kwamba mzigo uliobaki sasa hivi ni kwamba Rais Kikwete ameachiwa kama
mtu wa mwisho kufanya maamuzi juu ya azimio hilo.
Bunge lilipitisha maazimio manane
ikiwemo la kutenguliwa nyadhifa za Waziri wa Nishati na Madinii, Prof.
Muhongo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna
Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema, Wanakamati wa
Kudumu za Bunge hilo William Ngeleja (Sheria katiba na utawala), Andrew
Chenge (Bajeti), na Victor Mwambalasa.
Baada ya kamati kufanya maamuzi yake kazi imebaki kwa Rais Kikwete kufanya maamuzi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Kumekucha Blog
No comments:
Post a Comment