Jumatano December 24, kupitia kipindi cha XXL kumekucha blog, msanii TID,
amesikika akisema kuhusu Video yake mpya aliyoiachia ambayo
ameonekana kuvalia mavazi ya kiasili mavazi ambayo amesema ni ubunifu
wake mwenyewe kwa lengo la kuonyesha uhalisia wa Afrika, amesema kuvaa
vitu feki kwenye Video za mziki hakusaidii kupata mafanikio kwani
wasanii wanatakiwa watangaze tamaduni zao kwa kuziweka kwenye mziki
kama alivyofanya.Track hiyo mpya aliyoipa jina la Pressure tayari iko hewani na amemshirikisha msanii mkubwa kutoka Kenya, Nazizi , amesema ameamua kufanya na msanii huyo kutokana na uwezo wake mkubwa akiamini itafaya vizuri kutokana na kazi alizowahi kufanya nae kuweza kufika mbali ikiwemo kupata tuzo,
Akizungumzia mwaka 2014, Tid, amefunguka kuwa vitu vingi ambavyo alipanga kufanya kwa mwaka huu hakuweza kuvifanikisha ikiwemo kutoa Film yake mpya ya’Girlfriend Part Two’ kutokana na muda wa kuitengeneza na kuisambaza kuwa mdogo pamoja na bajeti kubana, Script ya film hiyo imeandikwa na marehemu George Tyson, ambae alikuwa awe director pia, miongoni mwa mastar watakao shiriki kwenye Film hiyo ni pamoja na Kalapina , Prof Jay, Ay, Monalisa, ambayo itafanyika mwakani.

Bonyeza play kusikiliza
Nitakufikishia kila story inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment