Saturday, December 6, 2014

Timua timua Somalia

Waziri Mkuu Somalia atimuliwa


mkuu wa taifa hilo Abdiweli Sheikh Ahmed mamlakani.
Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia.
Waandishi wanasema kuwa serikali ilikuwa imelemazwa na uhasama baina ya kiongozi huyo na rais wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.
Wanasema kuwa usalama ulikuwa umezorotoa kutokana na hali hiyo.
Abdiweli ni waziri mkuu wa pili kuwahi kuondolewa madarakani mwaka huu.
Marekani imeshtumu kura hiyo ikisema kuwa haikuzingatia maslahi ya raia wa Somali.CHANZO BBC

Kiongozi mwandamizi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda anayeshukiwa kupanga kulipuwa treni mijini New York na London ameuawa nchini Pakistan,kwa mujibu wa Jeshi la nchi hiyo.
Adnan el Shukrijumah aliuawa katika shambulizi kazkazini magharibi mwa Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan,jeshi hilo limesema.

No comments:

Post a Comment