Umeisikia hii ya mwanamke aliyemtupa mtoto dirishani akiwa kwenye basi?
Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka
amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za
kusababisha kifo cha mjukuu wake ambapo alimtupa mtoto huyo kwenye
dirisha la basi ambalo lilikuwa kasi, mwanamke huyo Waridi Saidi alimtupa mtoto huyo akiwa kwenye basi namba T 981 ALS la kampuni ya Salumu Classic lililotoka Dar kwenda Kigoma.
Mama huyo alimtupa mtoto huyo kijiji cha Iguguno, wilaya ya Mkalama alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshaki, Dk Adamu Hussein amesema
walimpokea mtoto akiwa katika hali mbaya kutokana na kuvuja damu nyingi
na siku ya pili alifariki dunia kutokana na jeraha la kupasuka kwa
fuvu la kichwa.
Lawaridi amesema; “dirisha
lilikuwa wazi yani nilimshusha tu nikamchukua Mayasa nikamtupa bila
kutegemea… Watu wakanivamia sasa huku wanapiga kelele kuanza kunipiga…
Wamenipiga sana tu, basi gari ikasimama wakawa wameenda kumtafuta mtoto…
nikaambiwa mtoto amepatikana lakini mpaka dakika hii sijamuona...“
Nimekuwekea hapa picha za kamanda wa polisi na mtuhumiwa akihijiwa na kituo cha ITV, hutopitwa na chochote mtu wangu na niko tayari kukupatia kila kinachojiri muda na wakati wowote, kupitia kumekucha blog
No comments:
Post a Comment