HABARI NDIO HIYO
***
BAADHI ya wanawake kutoka katika
Wilaya za Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya
ngono kinyume na maumbile.
Hayo
yalielezwa
na Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) wakati
akiwasilisha
utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na
maumbile
katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya
Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mremi
amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono
kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda
usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
“
Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na
kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar,
wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903
walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.
Aidha
alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa
wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5% huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufanhamu
njia hiyo ya kufanya mapenzi.
Wilayani
Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi
kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile
ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume
waliohojiwa
katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo kwaajili ya
kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na
wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya
mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai kupunguza raha
wanayo
ipata.
Wanawake
pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana
kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo
hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo
likichukua nafasi.
Watafiti
hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha
michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na
kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.
Aidha
imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa
wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili
kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa
wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito
mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.
Watafiti
hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia salama
za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na
maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.
Watafiti walioshiriki katika
utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth H Shayo,
Irene Mremi , Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson Kagaruki, Anjela Shija, Judith Msovela,
Dk. Leornad
Mboera,
Dk.Julius
Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana
Emid wote kutoka NIMR.