MATATIZO YA NDOA NA UMRI
MWANAUME MKUBWA ANAYEOA MSICHANA MDOGO
Imekuwa
ni kawaida katika jamii za kiafrika wanaume wenye umri mkubwa sana kuoa
wasichana wenye umri mdogo ambao wanaweza hata kuwazaa.Katika hili
imekuwa ni kama fashion kwa wasichana kiasi wamekosa hata zile haya
walizokuwa nazo wazazi wetu enzi za zamani.
Wasichana
wengi wametokea kujidumbukiza kuolewa na mababa wakubwa sana si
kuwa wanapenda kuolewa na wazee waliowazidi umri kwa kiasi
kikubwa.Wachache kati yao wanapenda kuolewa na watu wazima na wengi kati
ya hao hawapendi kabisa ndoa za namna hiyo na pia wengine hufuata pesa.
SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA WASICHANA WADOGO WALAZIMIKE KUOLEWA NA WANAUME WATU WAZIMA
Moja
ya sababu ambazo inapeleka wasichana wadogo kukubali kuolewa na wanaume
wakubwa waliowazidi umri sana ni Pesa,Sifa za majina ya wanaume jijini
au nchi walizopo,Umasikini wa familia walizotoka.hapo zamani wanawake
wengi waliolewa na wanaume kwa kukubali mapenzi ya dhati na kuzingatia
maadili mazuri ya ndoa.hawakuangalia suala la pesa au kuolewa na watu
wenye majina makubwamakubwa walipenda sana wanaume waaminifu na wachapa
kazi, wao pesa ilikuwa ni majaaliwa ya Mungu.
Wasichana
wa kileo wamekuwa na tamaa za harakaharaka kimaisha na kutopenda kabisa
kwenda kwenye ndoa yenye mashaka au dhiki za maisha.
Kila
msichana amekuwa akimtamani mwanaume yeyote yule mwenye pesa ili mradi
akafaidi maisha ya kileo na uhakika wa kila anachokiona kipya akipate.
Mabinti
wa kisasa hawapendi kujituma kama wale wa zamani ambao walikuwa
wakitwanga,wakichota maji,wakifua na hata kulima na kusaidia mifugo
pamoja na waume zao,siku hizi mtoto wa kike unamkuta hataki kucha zake
zikatike kwa kufua au kumsaidia mumewe kufua.
Wengi
wa wasichana wamekuwa na kasumba ya kuolewa na mwanaume yoyote yule
mwenye pesa ili kuondokana na umasikini wa familia zao bila kufanya
uchunguzi wowote ambao utaleta hathari katika ndoa zao.
MATATIZO YA NDOA NA UMRI (ATHARI)
Uchunguzi
nilioufanya katika wanandoa wengi toka jamii za kiafrika wanapatwa na
matatizo mengi ndani ya ndoa zao muda mchache tu mara ya kuingia katika
ndoa na watu wasiowafanyia uchunguzi wa kina kabla ya kukubali kuolewa.
Tukianzia
kwa upande wa wasichana ambao wamekuwa wakuimizwa sana na wanaume
waliokubali kuolewa nao kwa kufuata pesa ili kujikomboa kutoka hari
fulani ya kiwango cha chini kimaisha na kwenda huko kwa matajiri
wakifikiri watapata ahueni kwao.Au wale waliopenda kuolewa kwa kufuata
umaarufu wa wanaume wenye majina makubwa(Famours People).
Wanaume
wengi wanawalaghai wasichana wadogo kwa ahadi bandia [fake] pindi
wanapotaka kuwa nao,wengine uwapa magari kama zuga toto ili wakubali
kuolewa nao,wengine uwadanganya kwa kuwajengea nyumba.
(Athari namba Moja)
Wengi
wa wasichana wamezikwa kwa ukimwi kutokana na tamaa za kuolewa na
wanaume wakubwa hari ya kutaka maisha mazuri kwa kuona nikiolewa na
mwenye pesa nitaneemeka kimaisha.
(Athari namba mbili)
Wengine wameathirika kisaikolojia kwa kulazimika kukubali kuwa wake wenza hari ya kuwa hawakutarajia haya mwanzoni.
(Athari namba Tatu)
Kadhalika
wasichana wengi wamekuwa wakiteseka na ndoa zao kwa kutopata mapenzi
waliyotarajia na hii inatokana na wanaume wengi wenye pesa kukosa muda
wa kukaa na wake zao kutokana na shughuli za kazi zao zinavyowabana.
(Athari namba Nne)
Wengi
wa wanaume wenye pesa ni wahuni kiasi kwamba wanawatesa wasichana wengi
waliojiingiza bila kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuolewa nao.Na
matokeo yake wanabaki na simanzi kila kukicha kwa kushindwa kuondoka
kwenye ndoa wakifikiri watachekwa na wenzao au jamii inayomzunguka
kutokana na sifa walizozifuata wakizani watazikosa maishani…
Kwa leo tuishia hapa na fuatilia kesho kujua mambo mengi ya mahusiano ya mke na mume.
No comments:
Post a Comment