Kwa hii ndege unaambiwa New York mpaka London ni saa tatu tu !!
S-512 Supersonic Jet ndio ndege ambayo baada ya kunifikia Ripoti yake ilibidi nishtuke kidogo… eti New York Marekani mpaka London Uingereza ni safari ya saa tatu??
Nimepita mitandaoni ili kuangalia muda
wa wastani safari ya toka London mpaka New York kwa kawaida kabisa,
nimekuta ni mwendo wa saa saba mpaka nane.. mapinduzi haya hapa, kutoka
saa nane mpaka saa tatu !!
Spike Aerospace waliitambulisha
hii ndege kwa mara ya kwanza 2013, jamaa wameifanyia marekebisho ili
iwe salama zaidi kwa wasafiri, ndani ina uwezo wa kubeba watu 18 tu.
Nimeitafuta hesabu nyingine, umbali wa
toka New York mpaka London ni kama Kilometa 5,586 na hiyo ndege inatumia
saa tatu.. Safari ya Dar-Kigoma ni kama Kilometa 1,520, kwa maana hiyo
ni kwamba S-512 Supersonic Jet itasafiri toka Dar mpaka Kigoma kwa dakika kama 50 hivi.
Ninayo pia kwenye video hapa mtu wangu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment