HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Mkombozi Sanitarium Clinic, mabingwa wa tiba Asilia. Mkombozi wako na vipimo vya kupima mwili mzima na kutibu magonjwa sugu. Wanatibu Kisukari, magonjwa ya tumbo na homa za mara kwa mara. Wapo Chuda mkabala na Kampuni ya mabasi ya Raha leo. simu 0654 361333
NILIJUA NIMEUA 6
ILIPOISHIA JANA
Baada ya kulipeleka gari la
Dk Kweka katika gereji ya Habib niliondoka na kuendelea na shughuli zangu.
Uhusiano wangu na Mariam
ulizidi kukua. Alinibainishia jina lake
halisi
akaniambia anaitwa halima.
Ilifikia kutaka nimuoe akanikubalia lakini alinipa
masharti kwamba niwafukuze wapangaji wote kwenye nyumba yangu.
SASA ENDELEA
“Wafukuze wapangaji wote
halafu uikarabati hii nyumba” akaniambia.
“Unataka tuishi peke yetu?”
“Ndiyo. Sitaki kero. Chumba
kimoja uweke sebule”
“Kwa vile nakupenda nitafanya
hivyo”
Baada ya wiki moja
nikaufanyia kazi ushauri wa Halima. Niliwapa notisi wapangaji wote,
nikaikarabati nyumba na kuweka chumba kimoja kama
sebule.
Nilikuwa na shamba langu la
minazi. Fedha nilizopata kutokana na mauzo ya nazi zilinisaidia sana kukamilisha nyumba
yangu.
Halima aliendelea
kunitembelea mara kwa mara. Alipohakikisha nimetimiza matakwa yake akanielekeza
kwa wazazi wake nipeleke barua ya uchumba.
Wazazi wa Halima walikuwa
wakishi Pongwe, mwendo wa karibu kilometa kumi na tano kutoka Tanga mjini. Baba
yake Halima mzee Moto Bwagizo alikuwa mtu mzima sana. Niliambiwa kuwa Halima alikuwa mtoto
wake wa mwisho na alizaliwa bila kutegemewa kwani tayari baba yake alikuwa mzee.
Mama yake mzazi alishafariki.
Mzee Moto Bwagizo alikuwa na
wake wawili, mama yake Halima na mke mwingine. Baada ya kufariki mama yake
Halima, mzee Moto aliendelea kuishi na mke wake wa pili.
Niliwasilisha ujumbe wangu
kwa wazazi wa Halima. Baba mkwe aliponiona aliniambia hazitambui mila za kutuma
barua ya uchumba kwani mimi sikuwa nikiomba kazi. Ukiomba kazi ndio unatuma
barua.
“Mila ninazijua mimi za toka enzi na enzi ni za kutuma mshenga, anakuja na maneno tu”
“Samahani baba yangu, sikujua
ndio kama unanielimisha”
Mzee akacheka.
“Umenijibu vizuri. Sasa
fungua barua yako unisomee”
Nikafungua ile barua yangu na
kumsomea yale niliyoandika.
Mzee akafurahi akaniambia.
“Nimekuelewa. Unataka kuunga
udugu na sisi. Mimi kama baba wa Halima nakujibu hapa hapa kuwa nimekukubali.
Halima ni mchumba wako tangu sasa”
Mzee Moto alinitajia kiasi
cha pesa alichotaka ili aniozeshe binti yake.
Siku ya pili yake nilimchukua
rafiki yangu nikaenda naye kupeleka pesa hizo.
Mipango ya harusi ikafanywa.
Baada ya wiki mbili nikaenda
Ponwe kumuoa Halima.
Baada ya kuoana na Amina
ndipo nilipoanza kufaidi maisha ya ndoa. Kuse,ma kweli yalikuwa matamu kinyume
na kuishi kihuni.
Kwanza gharama ya maisha
ilipungua sana.
Pesa ambayo hapo mwanzo nilitumia peke yangu kwa siku kwa kula kwenye mikahawa, ilitumika kwa siku
mbili nilipokuwa na mke wangu.
Kadhalika nilikuwa na
mwenzangu wa karibu wa kuniliwaza, kunishauri na kunisaidia pale nilipohitaji
mwenza wa kunisaidia.
Kwa kweli nilihisi raha na
nilijilaumu kwa kuchelewa sana
kumuoa Halima.
Niliendelea na kazi yangu ya
teksi. Fedha nilizopata ntulitumia, kiasi kingine tuliwek kama
akiba yetu. Miezi michache tu baad ya kuoana, ndoa ilijibu. Halima akapata
ujauzito.
Halima alinijulisha usiku
kuwa alikuwa mjamzito. Wakati tunataka kulala aliniambia.
“Subiri”
“Nisubiri nini?” nikamuuliza.
“Subiri nikuoneshe kitu”
“Kitu gani?”
“Una haraka gani?”
Halima akasimama mbele yangu
na kuushika mkono wangu kisha akaushikisha kwenye tumbo lake chini
ya kitovu. Akawa anautomasisha kwenye tumbo lake.
“Unaona nini?” akaniuliza.
“Sioni kitu” nikamjibu.
“Huoni kitu kigumu gumu?”
“Nakiona, ni nini?”
Halima akauachia mkono wangu
kisha akapanda kitandani. Wakati anavuta shuka nilimuuliza.
“Mbona hukiambii ni nini?”
“Mimba!” akanijibu huku
akiendelea kijifinika.
“Hiyo ni mamba?”
Ndiyo”
“Mbona ndogo sana?”
“Si ndio inaanza, ina mwezi
mmoja. Ujue mwezi uliopita sikupata siku zangu”
Ni kweli ilikuwa mamba ya
mwezi mkmoja. Ilitupa furaha sote wawili. Tukaona karibuni tutaitwa baba na
mama.
Lakini kadiri siku
zilivyoendelea Halima alikuwa akiniambia anapolala usiku anaota ndoto
amejifungua watoro wawili mapacha. Watoto hao ni wazuri na weupe kama wazungu!
Nikadhani labda ni kweli
atajifungua mapacha. Mimba ilipoiza miezi mitatu Halima aliota akifanya tendo
la ndoa na mwendawazimu. Alipoamka akaanza kuumwa tumbo!
ITAENDELEA KESHO, usikose uhondo huu
No comments:
Post a Comment