Tuesday, July 7, 2015

BRAZILI NA MBINU MBADALA YA UFUNGUAJI KWA WANAWAKE

Uzazi wa upasuaji kupunguzwa Brazil

Sheria  mpya zinawalazimu madaktari kuwaarifu wanawake kuhusu hatari zilizopo na kuwashurutisha watie saini fomu za idhini yao kabla ya kuwafanyia upasuaji huo wakati wa kujifungua.
Madaktari hao pia watahitajika kutoa rekodi ya kujifungua kwa akina mama na kubainisha ni kwanini ilibidi wafanyie upasuaji.
Wanawake wengi Brazil hupendelea kuzaa kupitia upasuaji.
Katika hospitali za umma wanawake huona ndio njia salama na kwa walio na uwezo, wao huamua kuwalipa madaktari kando, kukwepa kukabiliwa na saa kadhaa za uchungu wa uzazi katika hospitali zilizo jaa wagonjwa.
Wanawake walio tajiri wanaokwenda katika hospitali za kibinafsi, wanaona upasuaji wakati wa uzazi ndio njia ya kisasa ya kujifungua.

No comments:

Post a Comment