Wednesday, July 15, 2015

CUF YAKANUSHA KUJITOA UKAWA


CUF yakanusha kujitoa Ukawa

 
  • Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magreth Sakaya alisema taarifa za wao kujitoa Ukawa ni za uzushi. Sakaya alisema CUF haikuweza kushiriki kikao cha jana kutokana na sababu za kikatiba ndani ya chama.


Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa zilizoenea kuwa kimejitoa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) .
CUF imesema kuwa haikuhudhuria katika kikao cha Ukawa kilichoendelea jana kwa sababu kwanza hawakupata taarifa na pia walikuwa na kikao cha ndani ya chama kama katiba yao inavyotaka.
Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magreth Sakaya alisema taarifa za wao kujitoa Ukawa ni za uzushi. Sakaya alisema CUF haikuweza kushiriki kikao cha jana kutokana na sababu za kikatiba ndani ya chama. “Katika chama chetu tunaendelea na vikao, maamuzi magumu ya chama huamuliwa na vikao vya juu vya maamuzi ndani ya chama,” alisema Sakaya.
Aliongeza kuwa Baraza Kuu la CUF litakutana Julai 25 kutoa maamuzi ili wanaposhiriki vikao vya Ukawa wawe kitu kimoja kama chama. “Maamuzi magumu ya chama huamuliwa na vikao vya maamuzi ndani ya chama, chama chetu kimekuwa kikiendelea na vikao vya ndani ili kuwa na maamuzi ya pamoja,” alisema. Ukawa jana walikuwa na kikao kilichodumu kwa takribani saa 14 na walitoa taarifa kuwa wameafikiana juu ya mgombea wa Ukawa hata hivyo atatangazwa baada ya siku saba.
Kwa habari ,matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment