Mama Kayai: Mzee Ojwang alipuuzwa
Mama Kayai ambaye ni mmoja kati ya wachekeshaji wa
vipindi maarufu vya Vitimbi na Vioja Mahakamani, ameuambia mtandao wa
Standard Digital kwamba Marehemu Ojwang, ambaye aliacha kuonekana kwenye
upeo wa wadau wa vichekesho mara baada ya kuanza kuugua macho mwaka
mmoja uliopita, alikuwa akilalama] siku za mwishoni mwa maisha yake,
lakini hakuna aliyekuwa akimfuatilia.
Nairobi, Kenya. Siku mbili
baada ya gwiji wa kuvunja mbavu kutoka Kenya, Benson Wanjau `Ojwang’
kuaga dunia katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, mchekeshaji mwingine
aliyekuwa akifanya kazi kwa ukaribu kabisa na Mzee huyo (kama mkewe),
Mary Khavere `Mama Kayai’, amesema ingewezekana kabisa kuokoa maisha ya
mzee huyo lakini alipuuzwa na hakuna aliyekuwa akisikia kilio chake cha
muda mrefu.
Mama Kayai ambaye ni mmoja kati ya wachekeshaji wa
vipindi maarufu vya Vitimbi na Vioja Mahakamani, ameuambia mtandao wa
Standard Digital kwamba Marehemu Ojwang, ambaye aliacha kuonekana kwenye
upeo wa wadau wa vichekesho mara baada ya kuanza kuugua macho mwaka
mmoja uliopita, alikuwa akilalama] siku za mwishoni mwa maisha yake,
lakini hakuna aliyekuwa akimfuatilia.
“Inauma sana kusikia huyu mzee ambaye ni baba wa
wachekeshaji nchini amefariki, lakini kinachouma zaidi ni kwamba mzee
ameomba sana msaada lakini hakuna ambaye alijitokeza mpaka alipofikia
hali mbaya zaidi”, alisema kwa masikitiko Mama Kayai.
Akionekana kuwa na hisia kali za majonzi alisema
ni watu wachache ambao leo wanaweza kujitokeza na kusema hawajawahi
kupata huduma nzuri ya vichekesho ya Mzee Ojwang lakini wengi wao
wamewahi kumuona na kumfurahia, ingawa katika siku za mwishoni mwa uhai
wake hakupata ushirikiano wa kutosha, kuokoa maisha yake.
Mzee Ojwang, amefariki bila ya kukutana ana kwa
ana na rais wake, Uhuru Kenyatta, mtu ambaye alikuwa akiomba na kuomba
itokee siku wakutane ili aongee naye japo kwa dakika chache.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Mzee Ojwang alipata tatizo
la macho na Seneta wa Jiji la Nairobi Mike Sonko alichukua jukumu la
kumpeleka Hospitali ya Loresho ambako alifanyiwa upasuaji na tatizo hili
lilisababisha gwiji huyo kupotea kabisa kwenye picha za runinga.
“Tangu hapo alikuwa katika hali nzuri tu na
alikuwa akiishi maisha ya furaha nyumbani lakini kwa kuwa hakuwa na
kazi, kuna wakati maisha yalikuwa magumu na akawa analazimika kuomba
msaada kwa jamaa”, alieleza mke wake, Augusta Wanjiru
Wanjiru alisema baada ya upasuaji, kiafya hakuwa
na hali mbaya ingawa jumatatu iliyopita, alianza kulalamika anaumwa
akawa anatapika mara kwa mara, hali ambayo wenyewe hawakuitilia
wasiwasi.
“Jumamosi usiku alianza kulalamika tumbo, na
ilipofika Jumapili ikabidi tumpeleke hospitalini na akakutwa na homa ya
mapafu na alifariki jioni yake,” alieleza mama huyo kwa masikitiko.
Binti yake, Patricia Njeri alisema kwamba mwili wa
baba yake, ulitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali
ya Taifa ya Kenyatta na kuhamishiwa katika vyumba vya kampuni rasmi ya
mazishi Kenya iitwayo Lee Funeral Home ya jijini Nairobi kusubiri
mipango ya mazishi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment