Ndoa za jinsia moja haziruhusiwi China, lakini hawa wamefunga!!
Siku chache zilizopita tulishuhudia Marekani wakihalalisha ndoa za jinsia moja kwenye majimbo yote, lakini hali haiko hivyo Beijing huko China, ndoa za jinsia moja zinakatazwa kisheria licha ya watu wengi kupinga Sheria hiyo.
Stori ya leo kutoka China inawahusu wanawake wawili wanaoishi jijini Beijing, Li Tingting na Teresa Xu waliyo
onekana kuto kujali Sheria ya nchi inayokataza ndoa za jinsia moja na
kuamua kufunga ndoa siku ya Alhamisi wiki iliyopita.
Wakiwa wapenzi wa muda mrefu, wadada hao
waliamua kufunga ndoa hiyo na kufanya sherehe kubwa iliohudhuriwa na
zaidi ya watu 50 siku hiyo ya Alhamisi kwenye moja ya hoteli huko
Beijing.
Wanandoa hao walisema walisukumwa kufanya maamuzi hayo kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Marekani wakisema walihisi muda umefika kwa wao pia kufunga ndoa baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu.
>>> “tunajua
sheria za nchi zinakataza, lakini kama Marekani wameweza kutambua kuwa
hata kundi la watu kama sisi tunastahili kutambulika kisheria hatuoni
sababu ya kwa nini watu waliopo huku wanyimwe haki hiyo, sheria
haitutambui na huwo ni uwonevu. <<< Li Tingting.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment