Tangakumekuchablog
Tanga,WATUMISHI
wapya wa Umma Tanga wametakiwa kuzingatia
maadili kazini pamoja na kuepuka vishawishi vya upokeaji rushwa
lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza juzi wakati wa kufunga mafunzo kwa watumishi wapya
kutoka vyuo mbalimbali Tanga , Mtendaji mkuu wa Tanroads, Patric Mfugale,
aliwataka wahitimu hao kuepuka kupokea rushwa na badala yake kufanya kazi kwa
weledi.
Aliwataka kuzingatia maadili pamoja
na kutoa ushirikiano kwa wananchi ikiwa na pamoja na kufika sehemu za kazi kwa
wakati na kukemea tabia ya baadhi ya watumishi kuchelewa sehemu zao za kazi.
“Leo niko nafuraha kuwa mgeni rasmi
hasa nikiwa mimi ndie nitakaekuwa mkuu wennu----niwambie kuwa sitomvumilia
mtumishi yoyote ambaye ni mtoro au mchelewaji sehemu ya kazi” alisema Mfugale
na kuongeza
“Kazi yangu kubwa ni kumuwajibisha
mtumishi atakaekuwa na makosa hasa ya kujihusisha na vitendo vya rusha----nitakuwa
mfuatiliaji mzuri kuanzia nidhani hadi mahudhurio” alisema
Mfugale aliwataka watumishi hao kuwa
mfano kwa watumishi wengine ikiwa na pamoja na kufanya kazi kwa bidii jambo
ambalo litaondosha manung’uniko kwa wananchi kupata huduma chini ya kiwango.
Awali akizungumza katika hafla hiyo,
Meneja wa mafunzo ambaye pia alikuwa kaimu mkurugenzi wa Tanroads tawi la
Tanga, Chales Mbuli, kuvaa mavazi yaendayo na utamaduni wa Kitanzania.
Alisema kuna baadhi ya watumishi
wake kwa waume wamekuwa wakienda maofisni na kuvaa nguo ambazo hazina heshima na
hivyo kushusha hadhi ya mtumishi mbele ya jamii.
“Ili kuwa watumishi wa kuigwa
nawaomba jambo la kwanza muvae mavazi ya heshima-----kuna baadhi ya watu
wanavaa nguo kama wanaenda disko au taarabu” alisema Mbuli
Ili kuweza kuleta ubunifu na
kuwasogezea maendeleo wananchi, Mbuli aliwataka watumishi hao kuwa wabinifu
katika kazi zao na kuacha kusema changamoto zinazowakabili .
Mwisho
Watumishi wa umma kutoka vyuo mbalimbali Tanga wakimsikiliza ,Mtendaji mkuu Taifa wa Tanroads, Patric Mfungale, wakati wa tafrija ya kuhitimu mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa Veta Tanga juzi
No comments:
Post a Comment