Tangakumekuchablog
Lushoto, MJUMBE
wa Baraza kuu la Taifa la Uongozi (UVCCM) Mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko, amesema
atajitosa kugombea nafasi ya Ubunge viti maalumu na kutoa ahadi kwa vijana
kumaliza kero zao zikiwemo fursa za mikopo na ajira.
Akizungumza mara baada ya kuchukua
fomu ya kugombea jana, Sekiboko alisema baada ya kufuatwa na watu wengi
wakiwemo vijana na wazee kugombea nafasi ya Ubunge viti maalumu ameamua kujitosa
kwa madai kuwa uwezo wa kuwatumikia yuko nao.
Alisema endapo atateuliwa kuwa
mbunge atahakikisha fursa za kupata mikopo na ajira kwa vijana zinapatikana ikiwemo
pia kuwajengea mbinu za uwezo za
biashara na kazi za mikono.
“Nimeshawishika kujitosa kugombea
nafasi ya ubunge baada ya kuombwa na matu wa marika tofauti---faraja zaidi
imekuja baada ya vijana wenzangu kunishinikiza na leo nimeamua kuchukua fomu”
alisema na kuongeza
“Niwahakikishie vijana wenzangu kuwa
sitowaangusha nikiwa bungeni kwani matatizo yenu nayaelewa juu chini-----niombeeni nifanikiwe kuwa mbunge wenu” alisema Sekiboko
Akizungumzia wanawake na vijana
kujitokeza kwa wingi katika nafasi za kugombea , Sekibko alisema wakati umefika
kwa makundi hayo kuacha kunung’unika kunyimwa haki zao na badala yake wajilaumu
wao wenyewe.
Alisema kuna wanawake wako na uwezo
wa kuongoza ila amedai kuwa wanashindwa kuchukua maamuzi na hivyo kuwataka uchaguzi mkuu mwaka huu kuonyesha mfano.
“Ni wakati wa makundi ya vijana
kujitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuacha kasumba huku tukilalamika pembeni kunyimwa
fursa-----ni sisi wenyewe ndio tunajiweka nyuma nyuma” alisema Sekiboko
Aliwataka vijana wake kwa waume
kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kusema kuwa kuna vijana wenye uwezo wa
kuongoza lakini wamekuwa wakijiweka nyuma nyuma na wengine hawajiamini.
No comments:
Post a Comment