Mke wa marehemu kazuiwa kwenye gari asiende kumzika mume wake! kisa kiko hapa…
Imetokea Shinyanga
ambapo wanafamilia pamoja na majirani walimzuia mke wa marehemu kwenda
kumzika mume wake kwa madai kuwa alikua akimnyanyasa enzi za uhai wake.
Wakati mume wake anafariki mama huyo
hakuwepo na alipopigiwa simu kuwa mume wake amefariki alirudi nyumbani
na kuwakuta ndugu wa mume wake na majirani wakiomboleza lakini yeye
akionekana kutojali na macho yakiwa makavu na hakuwa na dalili ya
huzuni.
Majirani wanasema aliwahi kumkana mume
wake tangu zamani pamoja na kumtesa huku akiishi na mume mwingine ambaye
ni mume wa mtu ndani ya nyumba ya mume wake huyo.
Wanandugu wa mume wakishirikiana na
majirani na Mwenyekiti wa mtaa walimshusha kwenye gari mama huyo na
watoto wake wakati wakienda kuzika kijijini kwao Bukoba na kuwaacha
wenyewe.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangaklumekuchablog
No comments:
Post a Comment