Msimamo wa Msumbiji uko kinyume na Afrika kuhusu ndoa za jinsia moja?
Ndani ya wiki moja tumeshuhudia
headlines nyingi kuhusu Marekani baada ya nchi hiyo kuhalalisha ndoa za
jinsia moja, leo ninayo nyingine iliyofikia kutoka Msumbiji!!
Kwao tangu mwaka 1886 ilikuwa MARUFUKU
kujihusisha na uhusiano wa jinsia moja, Jumatatu June 29 2015 Msumbiji
wametangaza kuhalalisha na kukubali kuzitambua ndoa za jinsia moja..
kingine kilichohalalishwa Msumbiji ni ishu ya wanawake kutoa ujauzito.
Marekani zilifanywa sherehe kubwa baada ya kuhalalishwa ndoa hizo, Msumbiji hakuna sherehe yoyote iliyofanywa mpaka sasa hivi.
Kuna nchi hawataki kabisa kusikia biashara ya kuhalalisha ndoa hizo, Rais Mugabe ni mmoja ya Marais ambao hawajifichi kabisa kupinga, Sudan, Nigeria na Mauritania
nako ukikamatwa hukumu yake ni kifo… Msumbiji imeamua hivyo japo
inaonekana nchi nyingi za Afrika zinapinga kuzitambua ndoa na uhusiano
wa jinsia moja.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment