Afrika Kusini kwenye headlines tena na mabadiliko ya Sheria!
Ulikuwa unafahamu ya kuwa kuna baadhi ya
nchi za Kiafrika haziruhushu vijana chini ya umri wa miaka 18 kufanya
mapenzi? Na adhabu yake mtu akikamatwa ni kifungo!?
Nimekutana na stori kutoka South Africa inayoweka headlines leo, South Africa hapo awali ilikuwa na Sheria iitwayo Sheria ya Makosa ya Jinai (Makosa ya Kujamiana na Mashirikiano) iliyokuwa inakataza vijana chini wa miaka 18 kufanya mapenzi.
Mwezi uliyopita Serikali ya South Africa ilifanya mabadiliko ya Sheria hiyo na Mwenyekiti wa Kamati Kwingineko juu ya Haki na Huduma za Magereza Mathole Motshekga alisema
hapo awali aliamini kuwa kama jamii jukumu lao ni kuwafundisha watoto
kujichunga, lakini alikuwa anakosea na kuwanyima watu hao haki zao za
kibinadamu.
Bunge la Katiba
lilikaa na kufanya mabadiliko juu ya vifungu 15 na 16 ya Sheria hiyo kwa
kusema kuwa Vifungu hivyo vinaenda kinyume na Katiba inayosema kila
Raia ana uhuru wa maamzi yake binafsi na pia ni kinyume na haki za
binadamu.
Bunge la Katiba
limesema kila mtu iwe mkubwa au mdogo ana haki ya kufanya maamuzi
binafsi yanayomhusu yeye bila kupingwa au kuingiliwa na mtu yoyote.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment