MGOMBEA URAIS KUTOKA TANGA , MUZZAMIL KALOKOLA NI MIONGOZI MWA WALIOSHINDWA KUREJESHA FOMU YA KUOMBA KUTEULIWA NAFASI YA URAIS
WATIA nia
wanne waliochukua fomu za kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kuwa wagombea wa kiti cha urais wametupwa nje ya mchakato huo,
baada ya kushindwa kurudisha fomu.
Walioshindwa
kurudisha fomu hizo mpaka muda wa mwisho ulipofika saa 10.00 jioni jana
ni Peter Nyalali, Helena Elinewinga, Anthony Chalamila na Dk Muzamil
Kalokola.
Mmoja wa
watia nia hao, Helena mara baada ya kuchukua fomu Juni 25, mwaka huu,
alikwenda kumtembelea mmoja wa maofisa wa chama hicho akitafuta ushauri
wa namna ya kufanya ili kupata udhamini, lakini baadaye aliamua
kutelekeza fomu hizo bila kuondoka nazo.
Jumla ya
wanachama 42 walijitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba uteuzi huo
ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini 450 kutoka mikoa 15, ikiwemo mitatu
ya Zanzibar.
Katika
mkutano wake na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Tanzania Bara, Rajab Luhwavi alisema zoezi la kuchukua fomu lilianza
Juni 3, mwaka huu na ulimalizika jana Julai 2 saa 10.00 jioni.
No comments:
Post a Comment