Bayern
Munich imeng’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya
kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani Munich, Ujerumani.
Atletico
Madrid imesonga kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa bao la
ugenini baada ya ushindi wa bao 1-0 ikiwa nyumbani Madrid.
Kusonga
mbele kwa Atletico Madrid, maana yake Kocha Pep Guardiola ambaye
anaondoka kwenda kujiunga na Manchester City, ameshindwa kutimiza ndoto
yake ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Bayern.
Mechi ilikuwa ngumu na tamu kuangalia na wenyeji walianza kupata bao katika dakika ya 31 kupitia Xabi Alonso.
Lakini Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico kabla ya Robert Lewandowski kuongeza la pili.
Kila
timu ilikosa penalti wakianza Bayern kupitia Thomas Muller na upande wa
Atletico, Fernando Torres naye akakosa, makipa wa timu zote wakiwa
mashujaa kwa kuzipangua.
Atletico
Madrid inasubiri mshindi kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City
katika mechi itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu
jijini Madrid.
No comments:
Post a Comment