Baada ya klabu ya Manchester City kumaliza msimu ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, kocha ambaye alikuwa anafundisha klabu hiyo Manuel Pellegrini ameweka wazi tatizo lililoifanya klabu hiyo kufanya vibaya msimu huu tofauti na msimu uliopita.
Manuel ameweka wazi kuwa kitendo cha uongozi wa Man City kuweka wazi kuwa klabu hiyo itakuwa na kocha mpya msimu ujao, kimechangia kudhoofisha timu, Guardiola alitangazwa na Man City kuwa atamrithi Pellegrini mwezi February, kitu ambacho kilifanya timu kupoteza morali katikati ya msimu.
“Nilitaka
kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, lakini uongozi wa
klabu ulipoamua kutangaza hadharani ujio wa kocha mpya, mambo yote
yalibadilika ikiwemo morali kwa wachezaji, tulipoteza mechi mbili muhimu
tukiwa nyumbani, wakati ambao tulikuwa tuna tofauti ya point tatu na
anae ongoza” >>> Pellegrini
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment