Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la
Polisi Mkoani Tanga, limekamata vifaa mbalimbali vya Ujambazi vinavyoaminika
kuwa vilikuwa vikitumika katika matukio ya Ujambazi yaliyotikisa jiji hilo na
kuuwa wateja wanne waliokuwa wakinunua bidhaa katika Duka la Supamarket.
Akizungumza na waandishi wa habari,
leo kamanda wa Polisi Leornard Poul, alisema vifaa hivyo vimekamatwa wakati wa
msako katika mapango ya Amboni kijiji cha Mleni ambako majambazi hayo yalikuwa
yamejificha.
Alisema majambazi hayo yaliyoaminika
kujificha katika mapango ya Mleni yalikuwa yakitumia silaha mbalimbali za jadi
pamoja na Bunduki pamoja risasi na miripuko.
Kamanda alisema wakati wa kuwasaka
majambazi hayo kulikuwa na kutupiana risasi ambapo majambazi manne walifanikiwa
kuwapiga risasi na kufa papo hapo ambapo askari wa wawili kujeruhiwa.
Akiwataja majambazi yaliopigwa
risasi na kufariki ni, Nassib Amir, Abuu Mussa, Abuu Katakoda pamoja na Idriss
Abdallah ambaye ametajwa kuwa ni Raia wa kigeni.
Kamanda Poul amewataja askari ambao walijeruhiwa kuwa ni ASP, Chale
na Inspector Gwanta Mwakisole.
Alisema majeruhui hao wanaendelea
kupata matibabu katika hospitali na hali zao zikiendelea viruhi na kusema kuwa
msako wa kuwasaka majambazi wengine unaendelea hivyo kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano na jeshi hilo.
Alisema Polisi kwa kushirikiana na
vikosi vya Usalama na Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kuwasaka majambazi hao
na kuahidi kuwatokomeza.
Mwisho
Pikipiki ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio ya Ujambazi zikiwa nje ya Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Tanga ambapo vitu mbalimbali vilikamatwa zikiwemo vocha za simu na simu pamoja na vifaa vya Elektonic .
No comments:
Post a Comment