Friday, August 26, 2016

SIKU YA MAOMBOLEZO YA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KUTAJWA

 Siku rasmi ya kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko la ardhi, Italy.

Mazishi ya kitaifa ya watu kadhaa yatafanyika Jumamosi
Siku ya kitaifa ya maombolezi imeanza nchini Italia, kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko kubwa la ardhi, lilokumba maeneo ya katikati ya taifa hilo.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi atahudhuria mazishi ya kitaifa ya waliouwawa katika eneo lililopata pigo kubwa, Arquata.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika maeneo yaliyoathirika.
Zaidi ya watu 280 wanaaminika kwamba wameaga dunia.
Takriban watu 400 kwa sasa wanatibiwa hospitalini.
Matumaini ya kupata watu wakiwa hai kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa yanafifia baada ya siku tatu za uokoaji.

No comments:

Post a Comment