Tuesday, August 30, 2016

WENGER AZIDI KUIBOMOA BENK YA ARSENAL

Wenger kasajili mshambuliaji mpya kwa zaidi ya Tsh bilioni 49

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimae leo August 30 2016 klabu ya Arsenal ya England inayofundishwa na kocha mfaransa Arsene Wenger imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania aliyekuwa anaichezea Deporivo La Coruna Lucas Perez.
Arsenal inaripotiwa kukamilisha usajili wa staa huyo na kumleta Emirates kwa dau la pound milioni 17.1 ambazo ni zaidi ya bilioni 49 za Kitanzania, Perez amejiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka minne.
Perez mwenye umri wa miaka 27 aliifungia Deportivo La Coruna magoli 17 katika mechi 37 msimu uliopita, hata  hivyo kocha Wenger anaripotiwa kujiandaa kutangaza kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea Valencia  Shkodran Mustafi dau linalofikia pound milioni 35.

No comments:

Post a Comment