Saturday, August 27, 2016

SOKONI MGANDINI TANGA



Takataka soko la Mgandini Tanga zikiwa zimerundikana nma kuzagaa hadi karibu na vibanda vya mama lishe na kusababisha harufu kali na wadudu wachafu kuingia maeneo yao na kuwa kero.
Mbali ya halmashauri ya jiji kulisafisha soko hilo kila siku jitihada zake zimekuwa zikirejeshwa nyuma na baadhi ya watu wasiozingatia usafi wa mazingira.
Baadhi ya watu waliozungumza na tangakumekuchablog wamesema elimu inahitajika ili kila mmoja kujua neo usafi wa mazingira.
Wamesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara na kaya majumbani zimekuwa zikitupa taka ovyo na kuzagaa hadi barabarani jambo ambalo limekuwa kero sugu.






No comments:

Post a Comment