Wednesday, August 31, 2016

MKUU WA WILAYA HANDENI GODWEN GONDWE AWATAKA WAKULIMA KULITUMIA SOKO LA (EAC)

 Tangakumekuchablog

Handeni, MKUU wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amewataka wakulima wa machungwa Wilayani humo kutafuta masoko nje likiwmo soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) kuepuka kulanguliwa na walanguzi wanaowafuata mashambani.
Akizungumza katika kikao mara baada ya kukabidhiwa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) kwa halmashauri ya Wilaya hiyo jana, Gondwe alisema wakulima wa machungwa  wanashindwa kuwa wakulima wa kisasa baada kushindwa kuthubutu kutafuta masoko nje.
Alisema soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki lipo lakini wanashindwa kulitumia badala yake wafanyabiashara wa nje huja mashambani kwao na kuwalangua kwa bei ya hasara.
“Kila mtu ndani na nje ya nchi wanajua kuwa Handeni inalima kilimo cha cha machungwa kwa wingi na wafanyabiashara huja , ila niwaambieni kuwa munalanguliwa kwa woga wa kwenda kutafuta masoko ” alisema Gondwe na kuongeza
“Soko la pamoja lipo wazi bila vikwazo vyoyote sasa ni kitu gani kinachotufanya kushindwa kulitumia na kuwaachia wenzetu kuja kwetu na kutulangua kwa bei ya kutupa hebu jamani tuondoe woga na tuwe tayari” alisema
Aliwataka wakulima kuacha woga na badala yake kuwa tayari kutafuta masoko ndani na nje ya nchi na kuwa wakulima wakubwa na kuacha kulanguliwa na wafanyabiashara mashambani ilhali fursa zipo.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Wafanyabiasha wa Machungwa Segera, Hussein Diamballa, aliwataka wafanyabiashara hao kucha kuuza machungwa yaliyopepewa na kusema kuwa kufanya hivyo kunaondosha sifa ya machungwa kituoni hapo.
Alisema kuna wachuuzi ambao wamekuwa wakiuza machungwa yaliyopepewa na kuchanganya mabovu na hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo kwani watafanya ukaguzi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema umoja huo uko mbioni kusajili wanachama ambao utakuwa na utaratibu wa kutoa namba na sare hivyo kuwataka kufanya biashara ya halali na kuacha udanyanyifu.
“Tunataka kuondosha ile dhana ya kituo chetu kuuza machungwa ya kupepea na kubambika mabovu, hii inatuletea sifa mbaya wakati hapa tunalima machungwa mazuri yenye maji mengi” alisema Diambala
Aliwataka wafanyabiashara hao kuwafichua wachuuzi wenye kufanya udanganyifu na kuwaletea sifa m,baya kwa wateja ilhali kituo hicho ni muunganisho wa magari yaendayo Mikoani jambo ambalo linaweza kuuza na kupata mitaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
                                            Mwisho



Wakulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga wakiwa katika semina ya kilimo cha machungwa na halizeti wakati wa kujadili andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
.

 Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Rajab Lusewa akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
 Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Bakari Mgaza, akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga, Said Msagati akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.

No comments:

Post a Comment