Mwanamume ameza visu 40 nchini India
Madaktari katika mji wa Amritsar kaskazini mwa India wamesema, wametoa visu 40 kutoka kwa tumbo la mwanamume mmoja.Daktari Jatinder Malholtra, ameambia BBC kwamba alikutana na mwanamume huyo wiki iliyopita alipokuwa akihisi maumivu makali kwenye tumbo lake.
Alisema mwanamume huyo hakuwafahamisha madaktari hao kwamba alikuwa akimeza visu.
No comments:
Post a Comment