Sunday, August 21, 2016

MUHONGO ATOA AGIZO ZITO KWA TANESCO


Tangakumekuchablog
Pangani,WAZIRI wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, ametoa agizo Tanesco Makao Makuu , Mikoani  na Wilayani kutoa elimu nyumba kwa nyumba  ili ifikapo mwaka 2020 kila nyumba inatumia nishati ya umeme.
Agizo hilo limekuja baada ya wananchi katika ziara yake ya kutembelea miradi ya usambazaji umeme Rea nchini kusema hawana elimu ya kutosha ya  umeme wa Rea .
Alisema Serikali imejiwekea malengo ifikapo mwaka 2020 kila Mtanzania anatumia umeme na Serikali kuuza nje ya nchi hivyo kuwataka Tansco kutoa elimu nyumba kwa nyumba lengo likiwa ni kupata elimu ya kutosha ya umeme wa Rea.
“Ndugu zangu natambua kuwa nyinyi ni wakulima wazuri  wa mbogamboga na matunda hapa kijijini, ushauri wangu  awamu hii ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili usiwapite kwani gharama zake ziko chini kabisa” alisema Muhongo na kuongeza
“Nyanya na mapapai pamoja na machungwa  nitafurahi kuona miongoni mwenu anawekeza kwa kufungua kiwanda cha kusindika matunda  na wakulima kuwa na soko la uhakika la kuuzia mazao yao” alisema
Aliwataka wananchi kuhakikisha  awamu hii ya pili  wa usambazaji umeme vijijini haupiti hivyo kila mmoja kutambua kuwa umeme ndio msingi wa maendeleo ya maisha ya kila mtu.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa jimbo la Pangani Jumaa Awesso, amewataka wananchi kuitumia fursa hiyo ya kupata umeme wa Rea ili kuongeza kipato.
Alisema ujio wa umeme huo utaweza kuwavuta wawekezaji hasa eneo la Mkalamo ambalo liko na  madini hivyo kusema kuwa fursa za maendeleo ziko nyingi mara baada ya kuingia majumbani.
Aliwataka wananchi hao  kuhakikisha fursa ya ujio wa umeme wa gharama nafuu haupiti na kuweza kufanya jitihada kwani baada ya hapo   gharama za kufungiwa umeme zitakuwa  juu na kuwa vigumu kwa mwananchi wa kipato cha chini kumudu.
                                                      Mwisho

No comments:

Post a Comment