Sunday, August 28, 2016

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI

Trump asisitiza kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji

Donald Trump amesema kuwa atajenga ukuta kuwazuia wahamiaji kutoka Mexico
Mgombea urais wa chama cha Rupublican nchini Marekani Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali kuwadhibiti wahamiaji.
Akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Iowa  Trump alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu ambao wanaishi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika.
Pia alirejelea wito wake wa kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico kuwazuia wahamiaji.
BBC

No comments:

Post a Comment