Thursday, August 25, 2016

WALIOFARIKI TETEMEKO LA ARDHI ITALIA WAONGEZEKA

Waliofariki Italia waongezeka, manusura watafutwa

Pescara del TrontoIdadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia mapema Jumatano imefika 247 huku manusura wakiendelea kutafutwa.
Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura na miili kwenye vifusi.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki.
Maafisa wa uokoaji waliendelea na juhudi za kuwatafuta manusura usiku, lakini wakati mmoja walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea na kutikisa majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Eneo lililokumbwa na tetemeko hilo ni milimani katika majimbo ya Umbria, Lazio na Marche.

No comments:

Post a Comment