Sunday, August 28, 2016

BIASHARA YA MUHOGO, LUMBESA

 WAPAGAZI, soko la Mgandini Tanga wakipakua roba la muhogo (Rumbesa) kwenye gari . Roba hilo lilikuwa likiuzwa 60,000.
Ujazaji wa Rumbesa umekuwa ukilalamikiwa na Chama Cha Utetezi wa usafirishaji mizigo na kusema kuwa ujazaji huo unawaumiza wakulima wadogowadogo.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Abrahman Shedaffa, alisema wamekuwa wakiwaeleza wakulima lakini kutokana na kutokuwepo kwa sheria wamekuwa hawajali.
Alisema kutokana na kukithiri kwa ujazaji Lumbesa chama hicho kitandaa mkutano mkuu wa wakulima na wafanyabiashara kulizungumzia suala hilo na kulikomesha.





Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment