Thierry Henry: Nyota wa zamani wa Arsenal apewa kazi Ubelgiji
Meneja
wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema nyota wa zamani
wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry, ambaye pia aling'aa sana
akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake.
Henry
alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu
Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi
hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mhambuzi wa soka kwenye Luninga.Nyota huyo huchambua soka katika Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport wakati wa Euro 2016.
Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.
No comments:
Post a Comment