Wednesday, August 24, 2016

ITALY YAKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI

Watu sita wafariki kutokana na tetemeko la ardhi Italia


Tetemeko la ardhiTetemeko la ardhi ItaliaTetemeko la ardhiTetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter limetikisa eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukua watu chini ya vifusi, maafisa wa Italia wamesema.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.
Mitetemeko ilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma na Italia. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica.

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika eneo la Accumoli, na meya wa mji jirani wa Pescara del Tronto amesema watu wawili wazee walifariki baada ya nyumba yao kuporomoka.
Eneo hilo, ambalo linapakana na mikoa ya Lazio na Marche, ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia.

No comments:

Post a Comment