Sunday, August 14, 2016

WAZIRI MUHONGO AWAPA SOMO TANESCO



Tangakumekuchablog
Lushoto, WAZIRI wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, amelitaka shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Tanga, kutoa elimu kwa wananchi vijijini juu ya umuhimu wa kuunganishwa umeme wa mradi wa Rea.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Wilayani hapa, Muhongo alisema kuna muitikio mdogo wa wananchi vijijini waliojitokeza kuomba umeme tofauti na malengo yaliyokusudiwa.
Alisema kuna baadhi ya maeneo yenye kaya zaidi ya 300 watu waliojitokeza kuomba umeme  hawazidi 100 hivyo upo umuhimu wa shirika hilo kufanya mikutano ya wananchi vijijini kutoa elimu ya umeme wa Rea.
“Tumepita maeneo mbalimbali na wananchi kusema hawajui wapi wananzia na nani wanamuona kuchukua fomu ya maombi, hivyo ni dhahiri kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi” alisema Muhongo na kuongeza
“Niwatake nyinyi tanesco kuhakikisha awamu hii ya pili ya usambazaji umeme vijijini inafikia malengo ili tukienda awamu ya tatu tuwe tumevuka malengo tuliyojiwekea” alisema
Profesa Muhongo aliwataka wananchi kuhakikisha fursa hiyo ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili wanaitumia ikiwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kila kaya mjini na vijijini anatumia nishati ya umeme.
Alisema ujio wa umeme huo ni fursa pekee ya kuongeza kipato cha mwananchi wakiwemo wakulima badala ya kwenda mjini kukoboa mahindi na kusindika matunda shughuli zote zinafanyika vijijini.
Alisema badala ya wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika matunda na mbogamboga  mjini wanaweza kuwafuata wakulima  mashambani na kuweza kupata unafuu na kuboresha kilimo chao na kuwa wakulima wa kisasa.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga,  Abrahman  Nyenye      alisema shirika hilo limekuwa karibu na wananchi pamoja na viongozi wa vitongoji na vijiji juu ya mradi wa usambazaji umeme vijijini .
Alisema muitiko wa wananchi ni mkubwa lakini kuna baadhi ya nyumba hazikidhi haja ya kufungiwa umeme kutokana na kuwa za nyasi hivyo kutoa elimu ya kuboresha numba zao na kuweza kupata umeme.
Alisema nyumba za nyasi Shirika hilo la Tanesco limekuwa likitoa maelekeo na elimu kuwataka kuboresha nyumba zao kwanza ili kuweza kupata kufungiwa umeme na kusema wengi wamekuwa wakifanya marekebisho.
                                              Mwisho



Wazee wa Mlola Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Abeid Othman (kushoto) , Rajab Saguti (kulia) wakimpa salamu Waziri wa Nishati na Madini , Sospeter Muhongo (katikati) kufikisha kilio cha  kwa Rais wa John Pombe Magufuli kuwa toka Uhuru hakuna Rais yoyote aliewahi kufika jimboni humo hivyo kumtaka kuwatembelea.

No comments:

Post a Comment