Monday, May 15, 2017

AJIOA BAADA YA KUKOSA MCHUMBA

Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaaMsichana ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami aliambia BBC .
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.

No comments:

Post a Comment