Monday, May 22, 2017

JE , WAJUA NDIZI HUIVISHA MATUNDA MENGINE

ndiziNi tunda linalopendwa sana na wengi lakini ndizi mara nyingi huwa hazitumiwi sana sana wakati wa kuandaa mchanganyiko wa matunda maarufu 'fruit salad', ambao unapangiwa kukaa kwa muda bila kuliwa.
Baada ya kutolewa maganda na kukatwakatwa, rangi yake hubadilika haraka kutoka manjano inayovutia na kuwa rangi ya kahawia, na mara nyingi huharibu matunda yale mengine yaliyochanganywa nayo.
Lakini sasa huenda mambo yakabadilika.
Baada ya miaka mingi ya kujaribu, kampuni ya Marks and Spencer imebuni njia ya kuweka ndizi zikiwa safi na za kuvutia hata zinapochanganywa na matunda mengine.
Lakini kabla hatujajifunza ujuzi huu, ni vyema tuelewe kwa nini ndizi huharibika haraka.

No comments:

Post a Comment