ZULIA LA FAKI
NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA
BABU 26
ILIPOISHIA
“Alikuambia hivyo?”
“Ndiyo. Kwa kweli nilishangaa
sana”
“Wewe ulimjibu nini?”
“Nilinyamaza kimya. Sikuwa na
jibu”
“Milizungumzia mahali pa
kukutana?”
“Ametaka tukutane Lux Hotel,
kule Masaki”
“Saa ngapi?”
Saa nne, asubuhi hii”
“Sasa acha tujiandae tuje
huko”
“Lakini Inspekta huu si
utakuwa ni mzuka wa Ummy? Amejuaje kuwa
tulifukua kaburi lake?”
“Hapo tutakapomkamata kila kitu kitajulikana”
Kama nitakutana naye ni
lazima niwe karibu na polisi, nilijiambia
kimoyomoyo.
SASA ENDELEA
“Sasa wewe wahi kufika hapo
heteli kabla ya saa nne umsubiri yeye” Inspekta aliniambia kwenye simu.
“Mimi ndiyo najiandaa.
Nitahakikisha ikifika saa tatu na nusu niko pale”
“Tafadhali usikae katika eneo
lililojificha. Tunataka tukifika tukuone. Kama mtakaa katika eneo la wazi la
hoteli itakuwa vizuri sana”
“Sawa”
Baada ya kumaliza kuzumngumza
na Inspekta Amour. Sikungoja ifike saa tatu na nusu, niliondoka
muda ule ule kwa gari langu.
Niliendesha kwa
mwendo wa taratibu huku nikiwaza.
Niliwaza kwamba endapo polisi watafanikiwa kumkamata yule msichana, kitendo
hicho kitafichua mengi yaliyojificha.
Mengi yaliyojificha ni pamoja
na mali za babu yangu ambazo zimekuwa ni kitendawili ambacho nimeshindwa
kukitegua.
Kingine ambacho kingefichuka ni
kuhusu Ummy mwenyewe ambaye mpaka muda
ule tulikuwa hatujui kama alikuwa ni mzuka au alikuwa binaadamu.
Wakati niko njiani Inspekata
Amour akanipigia simu.
“Umeshakwenda huko Masaki au
bado?” akaniuliza.
“Ndiyo niko njiani, ninakwenda”
“Ukifika tu utanipigia simu
kunijulisha kuwa umekaa sehemu gani”
“Lakini na nyie msichelewe
sana, msije mkamkosa. Mimi nimekubali kukutana
naye kwa sababu yenu”
“Usiwe na wasiwasi. Tayari
makachero watatu wameshatangulia huko”
“Sawa”
Inspekta akakata simu.
Haukupita muda mrefu
nikaingia Masaki. Niliutafuta ule mtaa uliokuwa na hoteli ya Lux, nilipoupata
nikalielekeza gari ilipokuwa hoteli hiyo.
Baada ya dakika tatu tu hoteli
hiyo ikawa upande wangu wa kushoto. Wakati
nakata kona kuelekea kushoto, simu yangu ikaita tena. Kwa vile nilikuwa katika mwendo wa taratibu niliichukua na kutazama
namba iliyokuwa inanipigia.
Nikaona namba
ya Ummy!
Wakati naipokea ile simu nikamuona
Ummy mwenyewe amesimama katikati ya njia mita chache tu mbele ya gari langu.
Alikuwa ameshika simu sikioni. Kumuona kwake kukanigutusha. Nikasema “Hello”
kwenye simu huku nimemkodolea macho.
Vile alivyokuwa amesimama
katikati ya njia, nilihofia kwamba ningeweza kumgonga kwa vile nilikuwa
nimeshamkaribia. Nikafunga breki kusimamisha gari.
“Utaona leo! Utaona leo!” nikaisikia
sauti yake ikisema kwenye simu.
Kumbe sikuwa nimekanyaga
breki. Nilichokanyaga ni pedali ya mafuta. Gari lilifyatuka na kumgonga Ummy.
Ummy akatoweka ghafla mbele ya macho
yangu. Badala yake nikaona nimegonga nguzo mbili za umeme zilizokuwa zimebeba
transfoma.
Mlipuko uliotokea hapo
ulinizibua masikio. Nakumbuka kwa mara ya mwisho niliona
moto mkali ukiwaka kama umeme. Hapo hapo
fahamu zikanipotea.
Sikuweza kujua gari langu lilisesereka
na kwenda upande gani lakini nilizisikia kelele za watu waliokuwa wakikimbia
huku na huko. Baadaye nilisikia king’ora ambacho ama kilikuwa cha gari la
zima moto au cha gari la hospitali kama si cha gari la polisi.
Nilikuja kuzinduka nikiwa
katika chumba cha hospitali. Nilikuwa
nimefungwa bendeji sehemu mbali
mballiza mwilli wangu kuanzia kichwani hadi miguuni.
Wakati nazinduka wauguzi na
daktari, walikuwa wakishughulika na mimi. Karibu yangu niliona polisi mmoja
alliyekuwa na bunduki.
“Oh umezinduka!” Daktari
alipoona nimefumbua macho aliniuliza.
Sikumjibu kitu. Bado nilikuwa
nikjiuliza nimefikaje pale hospitalli.
“Unajisikiaje?” akaendelea
kuniuliza.
Nikatikisa kichwa changu.
“Sijisikii vizuri. Mwili wote unaniuma” nikamwambia.
“Maumivu yako sehemu gani
zaidi?”
“Hizi sehemu zilizofungwa
bendeji zinaniuma sana”
“Kuna baadhi ya sehemu
umeshonwa baada ya kukatwa na vioo vya
gari na kuna sehemu nyingine
hazikushoneka, zina majeraha makubwa ya kukatwa na vioo” Daktaria akaniambia.
Nikanyamza kimya na kuanza
kuitafakari ile ajali.
“Tutakupatia tenbe za
kutuliza maumivu. Utajisikia
vizuri” Daktari akaniambia.
“Nitashukuru”
Mara nikamuona Inspekta Amour
akiingia katika chumba hicho.
Alipoona namtazama alimuuliza
daktari kama angeweza kuongea na mimi.
“Mnaweza kuzungumza” alipata
jibu kutoka kwa daktari.
“Pole sana” Inspekta akaniambia.
“Asante”
“Nini kimetokea pale”
“Kwa kweli palitokea kitu
kama miujiza….”
ITAENDELEA ksho usikose uhondo huu mtamu na mwanana hapahapa
No comments:
Post a Comment