MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati msimu wa mvua za
masika ukielekea ukingoni, wananchi wanatakiwa kufuatilia taarifa
zinazoendelea kutolewa ili kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa
zinazoweza kutokea.
Msimu wa mvua za masika ulianza Machi na zitamalizika Mei mwaka huu,
katika maeneo ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika
mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro na Manaya , Kaskazini, Pwani ya Kaskazini katika
mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na
Pemba.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA, Dk. Ladislaus
Chang’a, alilieleza Nipashe jana kuwa mvua hizo zimeendelea kupungua
wakati zikifikia ukingoni.
“Mvua zinaendelea kupungua, lakini matukio machache ya mvua kubwa
yanaweza kuwatokea, hivyo wananchi wanatakiwa kutufuatilia taarifa
tunazotoa ili kuchukua tahadhari ingawa zimepungua lakini hatuwezi
kusema zimeisha hadi msimu umalizike,” alisema.
Alisema katika maeneo hayo na yale ya kuzunguka Ziwa Victoria wanapata
mvua mara mbili kwa mwaka ambazo ni mvua za vuli na masika na kwamba kwa
mwaka huu zilikuwa kubwa.
Alisisitiza kuwa msimu wa mvua bado unaendelea, ingawa zinaelekea ukingoni na kwamba zinaendelea
mgblog
No comments:
Post a Comment