Wednesday, May 24, 2017

POLISI YANASA SILAHA HARAMU LIKIWEMO GOBORE



Tanga, JESHI la Polisi Mkoani Tanga limedai kukamata sila tano ikiwemo gobore moja wakati wa Operesheni maalumu ya kuwasaka wahalifu katika Wilaya ya Kilindi na Handeni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda Wakulyamba amesema kuwa masako huo ulifanywa kwa siku sita kwa ushirikiano na wananchi.
Amesema wakati wa operesheni hiyo inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza silaha za kienyeji pamoja na mitambo ya utengenezaji wa pombe haramu ya Gongo.
Kamanda Wakulyamba amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika maeneo yao ikiwa na pamoja na kuwafichua watengenezaji wa Gongo.





No comments:

Post a Comment