Zulia la faki 0655 340572
NILIKIONA CHA MTO URITHI WA
BABU 25
ILIPOISHIA
“Nimelikuballi hilo wazo. Kwa
hiyo atakaponipigia simu nitazungumza naye baada ya hapo nitakujulisha”
“Utakapotujuliasha,
tutafika mahali hapo haraka sana”
“Sawa. Inspekata”
Baada ya kuagana na Inspekta
huyo niliondoka hapo kituo cha polisi na
kurudi nyumbani. Kwa sababu ya yale mawazo ya Ummy kukaa kichwani mwangu wakati
wote, nilikuwa sipendi kutembea zaidi ya kukaa nyumbani kwangu.
Kwa sababu ya kiherehere,
nilipofika nyumbani nikampigia mimi.
Simu ya Ummy haikupatikana. Siku ile nilijaribbu kumpigia mara kadhaa lakini simu yake ilikuwa haipatikani.
Jioni yake Inspekta Amour alinipigia
simu akaniuliza kama Ummy alinipigia.
“Hajanipigia bado” nikamjibu.
“Na wewe umejaribu kumpigia?”
“Nimejaribu mara nyingi
lakini simu yake haipatikani”
SASA ENDELEA
“Sawa. Tuendeleaa kusubiri.
Ninaamini kuna wakati atakupigia au wewe
utapiga na utampata”
“Kunipigia ni laziama. Mara
nyingi hunishitukizia”
“Hata kama atakupigia usiku
wa manane, pangana naye mahali pa
kukutana halafu nipigie muda huo huo”
“Sawa Inspekta”
Inspekta huyo akakata simu.
Mpango huo wa polisi ulikuwa umenipa
matumaini. Mwanzo nilikuwa sitaki yule msichana anipigie simu lakini
baada ya polisi kuandaa mpango huo nilikuwa na hamu ya kuona Ummy ananipigia
simu.
Kila nilipopigiwa simu na mtu
mwingine nilikuwa nashituka nikidhani ilikuwa simu ya Ummy. Wakati wote simu
yangu ilikuwa mkononi ili iwe rahisi kuisikia inapopigwa.
Usiku ule uukapita bila kupigiwa simu na Ummy. Siku
iliyofuata nayo ikapita. Usiku wake Inspekta Amour alinipigia tena kuniuliza.
Nilifurahi alivyokuwa ananipigia kwani alikuwa ananipa moyo sana.
“Hajapiga bado?” akaniuliiza.
“Hajapiga lakini ninaamini
kwamba atapiga”
“Sawa. Tuendelee kusubiri”
Asubuhi ya siku ya tatu yake
nikaamshwa usingizini na mlio wa simu. Niliamka nikaishika simu yangu ambayo
nilikuwa nikiiweka mchagoni mwa kitanda ili iinapoita niweze kuisikia.
Nikayafikicha macho yangu kuondoa
ukungu wa usingizi kisha nikaitazama sikrini ya simu.
Alikuwa ni Ummy! Moyo ukanishituka. Nikainuka na kukaa kitandani kasha nikaipokea ile simu.
“Hello!” Nikasema kwa sauti
iliyoonesha wazi kuwa nilitoka usingizini.
“Natumaini umzima?” Sauti ya Ummy
ikasikika kwenye simu.
“Mimi mzima, sijui wewe”
“Mimi mzima tu. Mbona upo kimya?”
“Nimekupigia mara nyingi
lakini hupatikani”
“Si wakati wote ninaweza
kupatikana”
“Nimeshaamua kuwa tuukutane
mahali popote”
“Kwanini mmekwenda kufukua
kaburi langu?”
Moyo wangu ukapiga kwa
kishindo.
“Kaburi lako?” Nikamuuliza
kwa kubabaika.
“Mmelifukua juzi na kuutoa mwili
wangu!”
Moyo uliendelea kunipiga kwa
nguvu.
Akilini mwangu nilijiambia,
huu kweli ni mzuka. Amejuaje kuwa
tulifukua kaburi lake?
Nikajiuliza tena kama itakuwa
busara kukubali kukutana naye.
Mawazo ya kukutana na
msichana huyo yalinibadilika hapo hapo. Kwa kweli nisingeweza kukaa na kuongea
na mtu aliyekwisha kufa.
“Kwa kweli sikufurahi” Sauti
ya Ummy iliendelea kuniambia baada ya
mimi kuwa kimya.
Kikapita kimya kingine kabla
ya sauti hiyo kusikika tena.
“Umesema tukutane wapi?”
Ilinichukua muda kumjibu.
“Sema wewe tukutane wapi”
Kwa kweli sauti yangu sasa ilikuwa
imenywea. Ujasiri wote ulikuwa umeshanitoka.
“Tukutane kule hoteli,
Masaki”
“Hoteli gani?’
“Ile ambayo tulikutana mara
ya kwanza”
“Kule ni mbali sana. Kwanini
tusikutane katika hoteli iliyo karibu”
“Iliyo karibu na wapi?”
“Iliyopo hapa katikati ya
jiji”
“Nadhani Masaki kunafaa
zaidi”
“Lakini anagalia, usichukue
chumba. Tukutane mahali pa wazi”
“Mbona umebadilika?”
“Tukutane mahali pa wazi tu kwa
ajili ya mazungumzo yetu”
“Sawa, nitakufahamisha
utanikuta wapi”
“Saa ngapi?”
“Tufanye saa nne”
“Sawa. Utanijulisha”
Ummy akakata simu. Hapo hapo
nikampigia Inspekata Amour
“Yule msichana amenipigia
simu sasa hivi” nikamueleza Amour kwa pupa.
“Amekwambiaje?”
“Kwanza amenilaumu kwamba
tulikwenda kufukua kaburi lake na kuutoa
mwili wake. Ameniambia kwamba
hakufurahishwa na jambo hilo”
ITAENDELEA kesho hapahapa usikose uhondo huu mwanana
No comments:
Post a Comment