Tanga, SHEIKH wa Mkoa Baraza la Waislamu Tanzania
(Bakwata) Tanga Juma Liuchu, amewataka wafanyabiashara wa vyakula masokoni
kuacha kupandisha bei za bidhaa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa
Waislamu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Liuchu amesema Mwezi
wa Ramadhani ni mwezi wa machumo na baraka hivyo kuwataka kumuogopa Mungu ili
kuepuka kupata dhambi.
Alisema wafanyabiashara wengi hukitumilia kipindi cha mfungo
wa Ramadhani kwa kupandisha bei za vyakula hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo
na badala yake kuwapa unafuu wafungaji.
“Niwatake wafanyabiashara masokoni na madukani kuacha
kupandisha bei za vyakula, hebu tuogope kuingia katika dhambi na tuwape unafuu
wafungaji” alisema Liuchu na kuongeza
“Tamaa za pesa ndogo ndogo tena za muda mfupi zisitutoe
katika imani na tukawakomoa wafungaji na hili nitalifikisha katika tume ya
kudhibiti bei za bidhaa madukani” alisema
Alisema kipindi hiki cha mfungo wafungaji hutumia futari
nyingi za nafaka hivyo kuwaasa wafanyabiashara hao kutumia ubinadamu na kuacha
kuwalangua.
Katika masoko makubwa Ngamiani, Mgandini, Uzunguni na
Makorora Mwandishi wa habari hizi alitembelea na kujionea bei za bidhaa ikiwemo
tambi ilikuwa zikuzwa 2,000, kunde, 2,300, maharage 2,000, sukari 2,500 , nazi
800 na mchele ulikuw aukiuzwa 2,300 hadi 2,500.
Mwisho
No comments:
Post a Comment