Wednesday, May 31, 2017

MANCHESTER UNITED KLABU YENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI

Man United ndio klabu yenye thamani kubwa UlayaManchester United ndio klabu yenye thamani kubwa barani Ulaya ikiwa na thamani ya Yuro bilioni 3 kulingana na kampuni ya biashara ya KPMG.
Mabingwa hao wa kombe la Yuropa wanaongoza katika orodha ya thamani ya Kampuni ya KPMG, ikiwa mbele ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid na Barcelona.
Utafiti huo uliangazia haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja.
Katika utafiti huo uliofanyiwa timu 32, vilabu vya Uingereza vilitawala orodha hiyo vikijaza nafasi sita kati ya 10 bora.
Andrea Sartori ambaye ni mkurugenzi wa maswala ya michezo katika kampuni ya KPMG amesema kuwa kwa jumla thamani ya soka imekuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
''Huku hilo likielezewa kufuatia kuimarika kwa matangazo, operesheni za biashara za kimataifa, uwekezaji wa vifaa vya umiliki wa kibinafsi, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi mzuri ni vigezo muhimu vya ukuaji huo'', alisema.
Kuhusu haki za matangazo, ligi kuu ya Uingereza inaongoza ligi nyengine za Ulaya ijapokuwa ligi nyengine zimeweka mikakati kupigania mashabiki wa kimataifa.
Vilabu kumi bora vyenye thamani ya juu kibiashara
  • 1.Manchester United -Euro3.09bn
  • 2.Real Madrid - Euro2.97bn
  • 3.Barcelona - Euro2.76bn
  • 4.Bayern Munich - Euro2.44bn
  • 5.Manchester City - Euro1.97bn
  • 6.Arsenal - Euro1.95bn
  • 7.Chelsea - Euro1.59bn
  • 8.Liverpool - Euro1.33bn
  • 9.Juventus - Euro1.21bn
  • 9.Tottenham - Euro1.01bn
  • Duru: KPMG

No comments:

Post a Comment