Monday, May 8, 2017

SAMAKI MKUNGA

 Wavuvi katika bwawa la Mabayani Pande Mkoani Tanga wakimuonyesha samaki aina ya Mkunga waliemvua jana, Samaki huyo walimuuza kwa shilingi 10,000.
Bwawa la Mabayani ndio linalotegemewa kwa matumizi ya maji Tanga ambapo kwa sasa watu wanaoshukiwa kuwa wachimbaji wa madini kwenye vyanzo vya maji katika milima ya Amani Wilayani Muheza wamekuwa wakiyachafua hali ambayo Mamlaka ya maji safi na Majitaka ikipambana na kuhakikisha maji hayo hayachafuliwi.
Hata hivyo kwa uharibifu huo Mamlaka ya Maji safi na Majitaka imekuwa ikigharamika  kuhakikisha maji hayo licha ya kubadilika rangi hayana dhara kwa mtumiaji.
Tanga Uwasa imekuwa ikifanya ziara mara kwa mara katika vyanzo vya maji katika Milima ya Amani na kuwataka wachimbaji madini kuacha kuchimba kwa madai kuwa kipindi hiki cha mvua bwawa lake hupokea maji yenye rangi ya tope tope.



 Wazazi wakiwa na watoto wao wakivuka bwawa la Mabayani Pande kama walivyokutwa leo.





No comments:

Post a Comment