Luushoto, KUFUATIA mawe zaidi ya matano kufunga
barabara Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, fursa nyingi za vijana kujipatia kipato
ziomejitokeza ikiwemo kuvusha watu kwa pesa.
Mawe hayo yaliyoanguka usiku wa juzi baada ya mvua kubwa
kunyesha barabara haipitiki zaidi ya watembea kwa miguu ambao huongozwa na
vijana ili kuepuka kuzama ndani ya tope zilizomeza barabara ambayo iko na ukubwa zaidi ya kilometa 10.
Vijana hao waliobuni mbinu ya kujipoatia pesa wametengeza
njia za magogo na kusimamisha mawe ili watu waweze kukanyaga na kupita jambo
ambalo wengi wameliona kuwa ni jambo zuri nyenginevyo maafa zaidi yangeweza
kujitokeza.
Abushehe Shembilu amesema kwa siku hujipatia elfu 20,000 kwa
kuwatoza wasafiri kwa shilingi 500 kila mmoja japo wengine hutoa 200 hadi 100.
Amesema kutokana na wingi wa maeneo ambayo ni hatarishi kila
mmoja yuko na kiwango chake kutokana na eneo lake jinsi lilivyo hatarishi
ambapo amedai kituo chake ndio kibaya zaidi.
Amesema kuna vijana wengi ambao kuanzia asubuhi hadi usku
wamekuwa wakiwabebea mizigo kichwani na kuwafikishia jiwe la mwisho amedai hao
ndio wanaoingiza kipato kikubwa.
Shembilu amesema kutokana na kuwa hiyo ni kazi hajali
kutapakaa matope mwili nzima ambapo
ifikapo saa sita usiku hufunga kazi yeye na wenzake .
Kwa upande wa mama ntilie wajasiriamali hao wamekuwa wakiuza
chakula zaidi ya kilo kumi wali pamoja na ugali na huisha na wateja wakiwa
katika foleni ya kutaka chakula.
Asha Abrahman alie katika jiwe la pili lililofunga barabara
amesema ametoka Lushoto mjini kupiga kambi hapo na kusema kuwa biashara inaenda
vizuri na kuwa na matumaini ya adha hiyo itakapoisha ataweza kupunguza matatizo
ya nyumbani kwake.
“Mbali ya kuuza chakula chetu hapa katika jiwe la pili ya
maporomoko haya tumekuwa tukiuza chai na chakula kwa watu wanaoelekea Lushoto
na wengi wamekuwa wakiishia hapa kwa kuogopa kuruka viunzi” alisema Asha
Alisema kwa jinsi hali ilivyo mbaya uwezekano wa kuondoshwa
mawe hayo inaweza kuchukua zaidi ya wiki mbili kutegemeana na mvua kuacha
kunyesha.
Amesema endapo mvua itaendelea kunyesha maji kuacha kuporomoko
kutoka milimani baada ya wiki moja njia itaanza kupitika na kusema adha hiyo
imekuwa fursa kwa wajasiriamali na vijana wanaojituma.
No comments:
Post a Comment