Saturday, May 13, 2017

SIMULIZI, NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU SEHEMU YA 26

ZULIA LA  FAKI
 
NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU  26
 
ILIPOISHIA
 
“Alikuambia hivyo?”
 
“Ndiyo. Kwa kweli nilishangaa sana”
 
“Wewe ulimjibu nini?”
 
“Nilinyamaza kimya. Sikuwa na jibu”
 
“Milizungumzia mahali pa kukutana?”
 
“Ametaka tukutane Lux Hotel, kule Masaki”
 
“Saa  ngapi?”
 
Saa nne, asubuhi hii”
 
“Sasa acha tujiandae tuje huko”
 
“Lakini Inspekta huu si utakuwa ni mzuka wa Ummy?  Amejuaje kuwa tulifukua kaburi lake?”
 
“Hapo  tutakapomkamata kila kitu kitajulikana”
 
Kama nitakutana naye ni lazima niwe karibu na polisi, nilijiambia  kimoyomoyo.
 
SASA ENDELEA
 
“Sasa wewe wahi kufika hapo heteli kabla ya saa nne umsubiri yeye” Inspekta aliniambia kwenye simu.
 
“Mimi ndiyo najiandaa. Nitahakikisha ikifika saa tatu na nusu niko pale”
 
“Tafadhali usikae katika eneo lililojificha. Tunataka tukifika tukuone. Kama mtakaa katika eneo la wazi la hoteli itakuwa vizuri  sana”
 
“Sawa”
 
Baada ya kumaliza kuzumngumza na Inspekta Amour. Sikungoja ifike saa tatu na nusu,  niliondoka  muda ule ule kwa gari langu.
 
Niliendesha  kwa  mwendo wa  taratibu huku nikiwaza. Niliwaza kwamba endapo polisi watafanikiwa kumkamata yule msichana, kitendo hicho kitafichua mengi yaliyojificha.
 
Mengi yaliyojificha ni pamoja na mali za babu yangu ambazo zimekuwa ni kitendawili ambacho nimeshindwa kukitegua.
 
Kingine ambacho kingefichuka ni kuhusu Ummy mwenyewe ambaye mpaka  muda ule tulikuwa hatujui kama alikuwa ni mzuka au alikuwa binaadamu.
 
Wakati niko njiani Inspekata Amour akanipigia simu.
 
“Umeshakwenda huko Masaki au bado?”  akaniuliza.
 
“Ndiyo niko  njiani, ninakwenda”
 
“Ukifika tu utanipigia simu kunijulisha kuwa umekaa sehemu gani”
 
“Lakini na nyie msichelewe sana, msije mkamkosa. Mimi  nimekubali kukutana naye kwa sababu yenu”
 
“Usiwe na wasiwasi. Tayari makachero watatu wameshatangulia  huko”
 
“Sawa”
 
Inspekta akakata simu.
 
Haukupita muda mrefu nikaingia Masaki. Niliutafuta ule mtaa uliokuwa na hoteli ya Lux, nilipoupata nikalielekeza gari ilipokuwa hoteli hiyo.
 
Baada ya dakika tatu tu hoteli hiyo ikawa upande wangu wa kushoto. Wakati  nakata kona kuelekea kushoto, simu yangu ikaita tena.  Kwa vile nilikuwa katika  mwendo wa taratibu niliichukua na kutazama namba iliyokuwa inanipigia.
 
Nikaona  namba  ya Ummy!
 
Wakati naipokea ile simu nikamuona Ummy mwenyewe amesimama katikati ya njia mita chache tu mbele ya gari langu.
 
 Alikuwa ameshika simu sikioni.  Kumuona kwake kukanigutusha. Nikasema “Hello” kwenye simu huku nimemkodolea macho.
 
Vile alivyokuwa amesimama katikati ya njia, nilihofia kwamba ningeweza kumgonga kwa vile nilikuwa nimeshamkaribia. Nikafunga breki kusimamisha gari.
 
“Utaona leo! Utaona leo!” nikaisikia sauti yake ikisema kwenye simu.
 
Kumbe sikuwa nimekanyaga breki. Nilichokanyaga ni pedali ya mafuta. Gari lilifyatuka na kumgonga Ummy. Ummy akatoweka  ghafla mbele ya macho yangu. Badala yake nikaona nimegonga nguzo mbili za umeme zilizokuwa zimebeba transfoma.
 
Mlipuko uliotokea hapo ulinizibua masikio. Nakumbuka kwa mara ya mwisho  niliona  moto mkali ukiwaka kama umeme. Hapo hapo  fahamu zikanipotea.
 
Sikuweza kujua gari langu lilisesereka na kwenda upande gani lakini nilizisikia kelele za watu waliokuwa wakikimbia huku na huko.  Baadaye nilisikia  king’ora ambacho ama kilikuwa cha gari la zima moto au cha gari la hospitali kama si cha gari la polisi.
 
Nilikuja kuzinduka nikiwa katika chumba cha hospitali. Nilikuwa  nimefungwa  bendeji sehemu mbali mballiza mwilli wangu kuanzia kichwani hadi miguuni.
 
Wakati nazinduka wauguzi na daktari, walikuwa wakishughulika na mimi. Karibu yangu niliona polisi mmoja alliyekuwa na  bunduki.
 
“Oh umezinduka!” Daktari alipoona nimefumbua macho aliniuliza.
 
Sikumjibu kitu. Bado nilikuwa nikjiuliza nimefikaje pale  hospitalli.
 
“Unajisikiaje?” akaendelea kuniuliza.
 
Nikatikisa kichwa changu.
 
“Sijisikii  vizuri. Mwili wote unaniuma” nikamwambia.
 
“Maumivu yako sehemu gani zaidi?”
 
“Hizi sehemu zilizofungwa bendeji zinaniuma sana”
 
“Kuna baadhi ya sehemu umeshonwa baada ya kukatwa  na vioo vya gari na kuna  sehemu nyingine hazikushoneka, zina majeraha makubwa ya kukatwa na  vioo” Daktaria akaniambia.
 
Nikanyamza kimya na kuanza kuitafakari ile  ajali.
 
“Tutakupatia tenbe za kutuliza  maumivu.  Utajisikia  vizuri” Daktari akaniambia.
 
“Nitashukuru”
 
Mara nikamuona Inspekta Amour akiingia katika  chumba hicho.
 
Alipoona namtazama alimuuliza daktari kama  angeweza kuongea na mimi.
 
“Mnaweza kuzungumza” alipata jibu kutoka  kwa daktari.
 
“Pole sana”  Inspekta akaniambia.
 
“Asante”
 
“Nini kimetokea pale”
 
“Kwa kweli palitokea kitu kama miujiza….”
ITAENDELEA ksho usikose uhondo huu mtamu na mwanana hapahapa
 

No comments:

Post a Comment