ZULIA LA FAKI
NILIKIONA CHA MOTO URITHI
WA BABU 23
ILIPOISHIA
Kitu ambacho kilitushangaza
zaidi mimi na Inpekta Amour ni kuwa tarehe ile ile ya usajili wa mara ya pili
ndiyo tarehe hiyo hiyo ambayo Ummy alianza kunipigia simu. Kumbukumbu za
tarehe zilikuwa bado zipo kwenye simu
yangu.
“Sasa tunaomba utupatie namba
nyingine ambazo zilimekuwa zikiwasiliana na namba hii” Inspekata Amour akatoa
ombi jingine.
Msichana baada ya kuangalia
kwa makini alisema.
“Hii namba tangu
iliposajiliwa kwa mara ya pili rekodi yake inaonesha kuwa iliwasiliana na namba moja tu”
Alipoitaja namba hiyo ilikuwa
ni namba yangu mimi.
Amour akanitazama kwa
mshangao kabla ya kuuliza swali jingiine.
“Ilifanya mawasiliano mara
ngapi?”
“Mara tano”
SASA ENDELEA
Inspekta Amour akanigeukia
mimi.
“Mlifanya mawasiliano mara
tano?” akaniuliza.
“Nafikiri inaweza kufika mara
tano”
“Inaonekana kama aliifufua
namba yake ili kukupigia wewe tu”
“Sasa swali, katika kipindi
chote cha miaka mitano alichoacha kutumia hii namba alikuwa wapi?”
“Ndicho hicho kipindi
anachodaiwa kuwa alikufa lakini usajili wake unaonesha kuwa hakuwa amekufa
miaka mitano iliyopita kwani alikuja
mwenyewe kuifufua namba yake”
Wakati tukiwa garini tukirudi
kwa mzee Nasri, Amour aliniambia.
“Nina mashaka na madai kuwa
Ummy alikufa”
“Kwa hiyo wazo la kuwa ni
mzuka kama alivyoniambia yeye halina ukweli?”
“Mimi kama polisi siwezi kukubaliana na wazo
kama hilo”
“Pale kwao wanasisitiza kuwa Ummy alishakufa na hata
majirani niliowauliza wameniambia kuwa
Ummy alikufa kweli”
“Sasa kama Ummy alikufa kweli,
yule aliyekwenda kuisajili ile namba ni nani?”
“Ndiyo maana ninaliona wazo la huo mzuka linahitaji kufanyiwa
kazi”
“Hivi wewe unaamini kuwa mtu aliyekufa anaweza
kuibuka tena na kuwa mzuka?”
“lisemwalo lipo. Ni vizuri jambo hili lichunguzwe”
Tulipofika kwa mzee Nasri tulishuka kwenye gari. Mzee
Nasri hakuwepo barazani. Amour akabisha
mlango wa nyumba yake.
Mzee Nasri akatoka.
“Karibuni” akatuambia.
Safari hii alitukaribisha
sebuleni.
Baada ya kuketi Amour
alimwambia.
“Tumekwenda katika kampuni
ya simu tumeambiwa kuwa usajili wa ile namba ni wa mwanao Ummy”
“Inawezekana. Ile namba
aliisajili yeye mwenyewe”
“Tuliambiwa aliisajili kwa
mara ya kwanza miaka sita iliyopita. Baadaye alacha kuitumia kwa miaka mitano.
Hivi karibuni alikwenda kuifufua kwa sababu namba yenyewe ilikuwa imefutwa”
“Alikwenda kuifufua nani?” Mzee akauliza akiwa
amemkazia macho Inspekta Amour.
“Alikwenda kuifufua Ummy
mwenyewe. Tumeoneshwa kitambbulisho
chake na siku hiyo hiyo alimppigia huyu kijana”
“Hilo jambo haliwezekanai. Bado nasisitiza kuwa Ummy
amekufa… Ummy amekufa…”
“Mzee huwezi kufufua namba ya
mtu mwingine. Ni lazima uoneshe kitambulisho chako ili utambulike kuwa wewe
ndiye mwenyewe”
Niliona jasho likimtoka yule
mzee.
“Sijui niseme nini..!”
akajisemea peke yake.
“Itabidi tulifukue kaburi la
Ummy” Ispekata akamwambia.
Mzee akamkazia macho tena
Inspekta.
“Kwanini?”
“Kwa sababu kuna madai kuwa
Ummy hakufa. Na kama itathibitika kuwa
Ummy hakufa anaweza kukabiliwa na kosa
la jinai”
“Kama italazimika kuwa hivyo, mimi niko tayari kuruhusu kaburi lake lifukuliwe ili mtibitishe
kuwa mwannangu alikufa”
Mzee akanitazama kwa
kunilaani. Alikuwa kama
anayejiambia mimi ndiye niliyeyaleta yote yanayotokea.
Siku ya pili yake kikosi
maalum cha polisi kikiongozwa na Inspekta Amour kilipewa kibali na mkuu wa
polisi wa wilaya, cha kulifukua kaburi
la Ummy kwa madai kuwa Ummy
hakuwa amekufa.
Tulifika katika eneo hilo la
makaburi saa nne asubuhi. Mzee Nasri na familia yake walikuwa wamesimama
pembeni wakiangalia. Uso wa Mzee Nasri
ulikuwa umefadhaika. Kitendo cha
kufukuliwa kaburi la mwanawe kilikuwa kimemkera.
Mkewe na mdogo wake Ummy
wallikuwa na mawazo tofauti. Wao walitaka kaburi hilo lifukuliwe
ili wathibitishe ukweli wa mambo.
Kulikuwa na daktari kutoka hospitali
ya Muhimbili ambaye aliletwa kwa ajili
ya kuuchunguza mwili utakaopatikana
ndani ya kaburi hilo.
Kazi ya kulifukua kaburi hillo ilianza saa nee na dakika tano.
Kwa vile wafukuaji
walikuwa polisi wawili, baada ya nusu saa tu kaburi hilo likawa wazi.
Makaburi ya kiislkamu
yanakuwa na mfereji mwembamba unaolazwa mwili wa marehemu. Mfereji huo unaoitwa
mwanandani hufinikwa na ubao wakati marehemu anapozikwa.
Ule ubao ulikuwa umeshaanza
kuoza. Lakini sanda ya marehemu ilikuwa bado ipo ingawa ilikuwa imefubaa.
Polisi waliokuwa wamevaa
mipira waliutoa mwili huo na kuuweka juu ya kaburi kisha
wakaifungua ile sanda upane wa
kichwani.
ITAENDELEA kesho usikose Uhondo huu
No comments:
Post a Comment