Tanga, KLABU
ya Waandishi wa habari Tanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto Njiti
hospitali ya Mkoa wa Bombo ikiwa ni kuwakumbuka.
Akizungumza mara baada ya
makabidhiano, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Tanga, Hassan Hashim, amesema
jamii imewasahau watoto hao hivyo kuwataka wakumbukwe.
Amesema msaada huo ni pamoja na
sabuni, maziwa pamoja na Pempas na kuahidi kutoa msaada pale ambapo
itakuwa ikihitajika.
Amesema Klabu hiyo imekuwa ikijikita
katika mambo ya kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu na kusaidia huduma za kjamii
wakati wa majanga.
Akitoa shukurani zake Kaimu Mganga
Mfawidhi Mkoa, Goodkluck Mbwilo, amesema Klabu hiyo imefanya jambo la kuigwa na
kusema kuwa kundi la watoto njiti limesahauliwa.
Amesema msaada huo utatumika kama
ilivyokusudiwa hivyo kuwataka watu wengine wenye uwezo kutoa msaada kwa wakundi
mbalimbali hospitalini hapo wakiwemo wazee na watoto.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Tanga (TPC) Hassan Hashim (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi
Mkoa wa Tanga, Goodluck Mbwilo moja ya msaada wa maziwa, sabuni, pempasi na
unga wa ulezi kwa watoto njiti hospitali
ya Mkoa wa Bombo Tanga jana. Nyuma ni manesi wa hospitali hiyo.
Katibu wa Klabu ya Waandisi wa Habari Tanga (TPC), Anna Makange (kushoto) akimkabidhi mfuko wa pempasi Kaimu Mganga Mfawidhi Mkoa wa Tanga, Goodluck Mbwilo msaada uliotolewa na klabu hiyo kwa watoto njiti hospitali ya Bombo Tanga jana.
Mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanga, Hadija Baghasha akimkabidhi chupa ya moto Kaimu Mganga Mfawidhi Mkoa wa Tanga, Goodluck Mbwilo ikiwa ni moja ya msaada kwa iliyotolewa na klabu hoyo kwa watoto njiti hospitali ya Rufaa ya Bombo jana
No comments:
Post a Comment