Sunday, May 28, 2017

ARSENAL WENGER ADAI KUHUJUMIWA

Arsene Wenger amesema kuwa amehujumiwa sana msimu huuk KOCHA Mkuu wa Arsenal ametaja ukosoaji ambao amekuwa akipata msimu huu kuwa hujuma ambayo hatosahau.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 ankabiliwa na shutuma kali kutoka kwa mashabiki kwa kumtaka kuondoka katika klabu hiyo ambayo ameingoza tangu 1996.
''Sijali ukosoaji kwa sababu tunafanya kazi ya umma'', aliambia BBC kabla ya mechi ya fainali kati ya Arsenal na Chelsea katika uwanja wa Wembley.
''Ninaamini kuna tofauti kati ya kukosolewa na kuchukuliwa hali ambayo hairuhusu kwa mwanadamu''.

No comments:

Post a Comment