Monday, May 29, 2017

ARSENAL WENGER MGUU MMOJA NDANI MGUU MMOJA NJE

Kroenke (kulia) amewahi kumtaja Wenger kama kocha bora kwa klabu hiyoIdadi ya vikombe Wenger alivyofanikiwa kuvibeba akiwa ArsenalKocha wa Arsenal Arsene Wenger amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu ambapo mustakabali wa mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa.
Matokeo ya mkutano huo bado hayajawekwa wazi, lakini maamuzi yanabaki baina ya Wenger na Kroenke na yatategemea pia kikao cha bodi kitakachojadili suala hilo leo hii.
Bado haijajulikana kama Wenger ataongeza mkataba baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 21.
Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi mpaka hivi sasa.

No comments:

Post a Comment