Tumesikia kuhusu ajali nyingi za Bodaboda, hivi unajua ni hasara kiasi gani imetokana na ajali hizo?

Waziri wa Uchukuzi
Dk. Harrison Mwakyembe
amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za pikipiki na kugharimu
maisha ya watumiaji wa usafiri huo tangu Serikali ilipoidhinisha
matumizi ya vyombo hivyo mwaka 2009.
Waziri Mwakyembe amesema ongezeko hilo
limesababisha hasara ya shilingi trilioni tatu kutokana na matibabu kwa
majeruhi na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
“…
Kutokana na ajali hizo inakadiriwa kwamba Taifa limepoteza zaidi ya
shilingi trilioni 3.2 mwaka jana tuu… kwa maana ya uharibifu wa vyombo
vingine vya usafiri, uharibifu ya miundombinu , gharaza za matibabu na
bima, gharama za uokoaji na usimamizi, upotevu na uharibifu wa mali
kwenye magari husika na Sumatra nawaombeni sana hebu washirikisheni
wenzenu trafiki wale… Kamanda Mpinga anzisheni jamani uhusiano wa karibu
na waendesha pikipiki kupitia asasi yao hii sasa ya mafunzo hii ya
APEC… Hebu kuweni karibu sana... ”–
Waziri Mwakyembe
No comments:
Post a Comment