Kumekucha blog
Tanga,MKAZI wa kijiji cha Duga Horohoro Tanga, Mbito Dilima amejinyoga hadi
kufa kwa kutumia chandarua chumbani
kwake na kuacha ujumbe uliosomeka kulazimishwa kuoa mke usiemtaka haikubaliki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kaimu
kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea juzi
saa 2 usiku nyumbani kwao na kuacha
ujumbe uliosomeka kulazimishwa kuoa mke nisiemtaka sikubali.
Alisema uchunguzi wa
awali wa kipolisi umebaini kuwa marehemu alichukua uamuzi wa kujinyonga baada
ya wazazi wake kumlazimisha kumuoa binti asiemtaka na kwa kipindi kiefu
akilikataa na kuzusha mgogoro ndani ya familia.
“Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa marehemu
alijinyonga hadi kufa kwa kutumia chandarua chumbani kwake na kuacha ujumbe
uliosomeka kulazimishwa kuoa mke nisiemtaka haikubaliki” alisema
“Ujumbe ule alikuwa ameuweka sikio la kulia kama wale wavuta
sigara na ukiwa ameukunja----kwa sasa tunakamilisha uchunguzi na maiti
tumeihifadhi hospitali ya Bombo” alisema Ndaki
Ndaki alisema polisi inaendelea na uchunguzi na inawahoji wazazi
wa marehemu pamoja na majirani wakati wakiendelea na taratibu za mazishi na
kutoa wito kwa wazazi kuwa na mahusiano mazuri kwa watoto wao kuepusha matukio
mabaya.
Katika tukio jengine, Ndaki alilitaja kuwa Mfanyabiashara wa
pikipiki (bodaboda), Juma Said alinusurika kuuwawa na watu wanasadikiwa kuwa ni majambazi baada ya
jaribio lao la kumteka kushindikana.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6 usiku maeneo ya
Magomeni Tanga baada ya watu hao
waliokuwa watatu kupakia mishkaki na walipofika katika eneo lenye mchanga mwingi walimuamuru kuachia
pikipiki .
Alisema wakati wakibisha kwa maneno na kutishia kupigana
mmoja wa majambazi hao alitoa sime na kumtaka aondoke zake vyengine watamkata
mikono na miguu.
“ Wale majambazi walikuwa watatu na walitoka nae mjini na
walikubaliana vizuri tu---walimpa elfu kumi na tano ili akubali kwani gharama
yake kwa uhalisia ni elfu nne” alisema Ndaki
“Kila siku polisi imekuwa ikiwaeleza bodaboda kuwa na
utaratibu wa kujiwekea muda wa kikomo cha kufanya kazi----wako na masikio
yasiosikia dawa na matokeo yake ni kama haya” alisema Ndaki
Alitoa wito kwa madereva hao kuwa na umoja na kufanya
mawasiliano katika vituo vyao hasa anapotokea mmoja wao kukodiwa nje ya mji
hasa nyakati za usiku ambazo zimekuwa
zikitumiwa na watu wabaya.
No comments:
Post a Comment